Lugha Nyingine
Bei za walaji za China zadumisha kupanda kwa kasi ya wastani mwezi Julai (3)
![]() |
| Mwanamke akinunua mafuta ya kupikia kwenye supamaketi, Mengzi, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Agosti 9, 2026. (Picha na Xue Yingying/Xinhua) |
BEIJING - Bei za walaji za China zimedumisha ongezeko la wastani kwa ujumla mwezi Julai, zikionyesha nafasi ya kutosha kwa kuanzisha sera zinazohimiza matumizi katika nusu ya pili ya mwaka.
Fahirisi ya bei za watumiaji (CPI), kipimo kikuu cha mfumuko wa bei, kilipanda kwa asilimia 0.5 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana mwezi uliopita nchini China, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) jana Jumapili. Takwimu hizo zinaonesha kuwa CPI kuu, ambayo haijumuishi bei za chakula na nishati, iliongezeka kwa asilimia 0.9 kutoka mwaka jana kipindi kama hicho.
“Ongezeko hilo la CPI kutoka mwaka jana linapungua kwa asilimia za pointi 0.5 kuanzia Juni, hasa kutokana na ongezeko la polepole la bei za petroli,” amesema Dong Lijuan, mtaalamu wa takwimu wa NBS, akiongeza kuwa bei za petroli zilipanda kwa asilimia 1 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, huku kiwango cha ukuaji kikishuka kwa asilimia za pointi 16 kutoka mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa NBS, bidhaa za matumizi za viwandani bila kuhusisha nishati ziliongezeka kwa asilimia 1.5 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, zikipungua kwa asilimia za pointi 0.2 kutoka mwezi uliopita, zikichangia asilimia za pointi takriban 0.37 katika ukuaji wa CPI.
Imesema bei za huduma ziliongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, ikiwa ni kushuka kwa asilimia za pointi 0.1 kuanzia Juni, zikichangia asilimia za pointi takriban 0.36 katika ukuaji wa CPI. Bei za chakula zilishuka kwa asilimia 1.5 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, zikipunguza kushuka kwa asilimia za pointi 0.1 kutoka mwezi uliopita, na kushusha CPI chini kwa asilimia za pointi takriban 0.25.
Kwa kipimo cha kutoka mwezi mmoja hadi mwingine, CPI ilishuka kwa asilimia 0.1 mwezi Julai, huku kupungua kwake kukishuka kwa asilimia za pointi 0.2 kutoka mwezi uliopita, kwa mujibu wa NBS.
NBS imesema bei za chakula zilidumisha viwango vilevile kutoka mwezi mmoja hadi mwingine, asilimia 0.6 chini ya wastani wa msimu. Bei za huduma, ambazo pia hazikubadilika mwezi Juni, zimebadilika na kuwa ongezeko la asilimia 0.4 kwa mwezi, na kuongeza CPI kwa asilimia za pointi takriban 0.21.
“Kuna nafasi kubwa kwa sera za kuhimiza matumizi katika nusu ya pili ya mwaka, na hasa mambo ya bei hayatakuwa kizuizi kikubwa kwa uwezekano wa benki kuu kupunguza riba,” amesema Wang Qing, mchambuzi mkuu wa uchumi wa jumla katika Golden Credit Rating.
Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hivi karibuni ilifanya mkutano kuhusu kazi ya uchumi, ambao ulisisitiza hitaji la kupanua mahitaji ya ndani kwa ufanisi, kuongeza usambazaji wa bidhaa na huduma zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya makundi tofauti, na kutumia kikamilifu uwezekano wa matumizi ya huduma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




