Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa Mashindano ya 48 ya Ufundi Duniani

(CRI Online) Septemba 23, 2026

Rais Xi Jinping wa China jana ametuma barua ya pongezi kwa Mashindano ya 48 ya Ufundi Duniani.

Rais Xi amesema, hivi sasa duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na viwanda inaongeza kasi, ikileta athari kubwa kwa maendeleo ya ufundi duniani. Mashindano ya ufundi duniani yanaungana kwa karibu na mahitaji ya viwanda, na kutoa jukwaa zuri la kufunzana kati ya watu wenye vipaji vya ufundi kutoka nchi mbalimbali.

Rais Xi amesisitiza kuwa, China itatumia mashindano hayo kama fursa ya kuongoza wafanyakazi wengi zaidi hasa vijana kuelekea njia ya kujiendeleza kwa ufundi.

Pia Rais Xi amesema China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na pande mbalimbali, ili kuhimiza maendeleo ya mashindano ya ufundi duniani, na kuhudumia vyema zaidi ukuaji wa uchumi wa dunia na kuboresha maisha ya watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha