Lugha Nyingine
Rwanda na China zarejea ahadi ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili
Rwanda na China zimerejea ahadi yao ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili wakati Ubalozi wa China nchini Rwanda ukisherehekea maadhimisho ya miaka 77 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Hafla ya maadhimisho hayo, iliyofanyika jioni ya Jumanne jijini Kigali, mji mkuu wa Rwanda, iliwakutanisha wawakilishi kutoka serikali ya Rwanda, ujumbe wa kidiplomasia, wasomi, vyombo vya habari na jamii ya Wachina.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Usta Kaitesi ameipongeza China kwa maadhimisho hayo na kusifu mafanikio yake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sayansi na teknolojia, pamoja na miundombinu.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Rwanda Gao Wenqi amesema kuwa urafiki kati ya China na Rwanda umeendelea kuimarika tangu mwaka 1971, hasa kufuatia kupandishwa kwa ngazi ya uhusiano wa nchi hizo mbili hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati wa kina mwaka 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



