Mwogeleaji kijana wa China, Yu apata medali tatu, Korea Kaskazini yatawala kwenye mchezo wa kuinua uzito

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 24, 2026

Yu Zidi wa China akipiga picha baada ya kushinda fainali ya mchezo wa kuogelea mita 400 kwa wanawake katika Michezo ya Asia ya 2026 huko Tokyo, Japan, Septemba 23, 2026. (Xinhua/Wu Zhizun)

Yu Zidi wa China akipiga picha baada ya kushinda fainali ya mchezo wa kuogelea mita 400 kwa wanawake katika Michezo ya Asia ya 2026 huko Tokyo, Japan, Septemba 23, 2026. (Xinhua/Wu Zhizun)

Mwogeleaji wa China mwenye umri wa miaka 13, Yu Zidi, jumatano alifanikiwa kupata medali tatu kwenye mashindano ya Michezo ya Asia ya 2026, huku Korea Kaskazini ikifungua ukurasa wake wa medali ya dhahabu kutokana na wanyanyuaji wa uzito wa kike.

Yu aliendelea kuonesha uhodari wake katika Michezo hiyo ya Asia, kwa kujipatia medali yake ya tatu ya dhahabu kwa kushinda medali ya wanawake kwenye mashindano ya kuogelea mita 400, baada ya ushindi katika mchezo wa mita 200 za kipepeo na mita 200 mtindo mchanganyiko. Aliongoza hadi mwisho na kuweka rekodi ya Michezo hiyo ya Asia kwa kutumia muda wa dakika 4:28.56.

"Nimepata mengi kutokana na Michezo hii ya Asia lakini pia kulikuwa na majuto," alisema.

Zhang Yuning (mbele) akionyesha kidole gumba baada ya sare ya 0-0 kati ya China na Falme za Kiarabu katika Michezo ya Asia ya 2026 huko Toyota, Japan, Septemba 23, 2026. (Xinhua/Jia Haocheng)

Zhang Yuning (mbele) akionyesha kidole gumba baada ya sare ya 0-0 kati ya China na Falme za Kiarabu katika Michezo ya Asia ya 2026 huko Toyota, Japan, Septemba 23, 2026. (Xinhua/Jia Haocheng)

China imefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya mpira wa miguu kwa wanaume ikiwa mshindi wa kundi, baada ya kupata sare ya 0-0 dhidi ya Falme za Kiarabu katika mechi yake ya mwisho ya makundi.

Wang Chuqin, Lin Shidong na Wen Ruibo wa timu ya China (Kushoto hadi Kulia) wanaingia uwanjani kabla ya mchezo wa nusu fainali wa timu ya wanaume kati yake na timu ya Taipei ya China katika Michezo ya Asia ya 2026 huko Toyota, Septemba 23, 2026. (Xinhua/Cheong Kam Ka)

Kwenye mchezo wa nusu fainali ya mpira wa meza, timu ya wanawake ya China imefuzu fainali baada ya kuishinda timu ya Korea Kaskazini kwa seti 3-0. Timu ya wanaume vilevile imeishinda timu ya Taipei, China kwa seti 3-0, na kujiandaa kwa mchezo wa kugombea medali ya dhahabu kati yake na timu ya nchi mwenyeji Japan. Wakati huo huo, wachezaji wawili mchanganyiko Wang Chuqin na Sun Yingsha wamewashinda Feng Yi-hsin na Yeh Yi-tian wa timu ya Taipei, China kwa seti 3-0.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha