Utalii washamiri kwenye Mfereji wa Pinglu katika Mkoa wa Guangxi, kusini mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2026
Utalii washamiri kwenye Mfereji wa Pinglu katika Mkoa wa Guangxi, kusini mwa China
Watalii wakiwa wamepanda boti za utalii katika eneo la huduma za njia ya maji kwenye Mfereji wa Pinglu, Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Septemba 29, 2026. (Xinhua/Zhou Hua)

Katika siku za hivi karibuni, utalii umekuwa ukishamiri kwenye Mfereji wa Pinglu katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. Watalii wengi hupanda boti za utalii ili kutazama njia za maji, vituo vya usafiri wa majini na madaraja ya mfereji huo, na kufurahia mandhari kando yake.

Mfereji huo wa Pinglu, ambao ulifunguliwa rasmi kwa usafiri wa majini Septemba 16, unaunganisha njia ya usafiri wa meli ya Mto Xijiang na Ghuba ya Beibu, na ni kiungo muhimu kinachounganisha njia za maji za ndani ya bara ya China na bahari.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha