Michezo ya Asia | China yashinda medali ya dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti za mita 100x4 kwa wanariadha wa kike na kiume

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2026
Michezo ya Asia | China yashinda medali ya dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti za mita 100x4 kwa wanariadha wa kike na kiume
Shi Junhao, Liu Guoyi, Chen Yujie na Chen Jinfeng (kutoka kushoto kwenda kulia) wa China wakishangilia baada ya fainali ya mbio za kupokezana vijiti za mita 100x4 kwa wanamichezo wa kike na kiume kwenye Michezo ya 20 ya Asia ya Aichi-Nagoya 2026, Nagoya, Japan, tarehe 29 Septemba 2026. (Xinhua/Lui Siu Wai)

NAGOYA, Japan - China imeshinda medali ya dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti za mita 100x4 kwa wanariadha wa kike na kiume kwenye Michezo ya Asia ya Aichi-Nagoya jana Jumanne, ambapo timu hiyo ya wanariadha wanne—Chen Jinfeng, Liu Guoyi, Shi Junhao na Chen Yujie—imemaliza mbio hizo kwa muda wa sekunde 40.78. Thailand imeshinda medali ya fedha na India imepata medali ya shaba.

Hiyo ni medali ya tatu ya dhahabu kwenye michezo hiyo kwa Chen Yujie, ambaye tayari alikuwa ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 kwa wanariadha wanawake na mbio za kupokezana vijiti za mita 100x4 kwa wanariadha wanawake, pamoja na medali ya fedha katika mbio za mita 200.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha