Lugha Nyingine
Mcheza tenisi wa China Zheng Qinwen afuzu kwa nusu fainali ya China Open (4)
BEIJING – Mcheza tenisi Zheng Qinwen wa China amefuzu kwenda nusu fainali ya michuano ya China Open kwa upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja dhidi ya mmoja jana Ijumaa, akimshinda mchezaji wa nafasi namba 6 ya mashindano hayo Elina Svitolina wa Ukraine kwa seti 6-3, 7-6(6) katika siku yake ya kwanza baada ya kufikisha umri wa miaka 24.
Akicheza na mpinzani wake wa kwanza wa nafasi 10 bora za mashindano hayo, Zheng alishinda pointi wakati mpinzani wake kuanzisha kupiga mpira mara tatu katika seti ya kufungua mechi. Alishinda pointi wakati mpinzani wake akianzisha kupiga mpira katika seti ya kwanza na ya saba, lakini akajikuta na yeye pia akishindwa wakati wa kuanzisha kupiga mpira kwa seti 5-3, kabla ya kupata ushindi wake wa pointi wa tatu wakati mpinzani wake akianzisha kupiga mpira katika seti ya tisa na kuhitimisha kwa kuongoza seti 6-3.
Svitolina alipandisha kiwango chake katika seti ya pili na kumshinda pointi Zheng wakati akianzisha kupiga mpira katika seti ya saba na kusonga mbele kwa seti 4-3, na baadaye mchezaji huyo Mchina alijibu mapigo mara moja katika seti ya nane. Wachezaji wote wawili walishikilia nafasi ya kuanzisha kupiga mpira ili kulazimisha ushindi wa pointi kuamua mshindi baada ya sare, ambapo Zheng alikuwa nyuma kwa 0-2 kabla ya kushinda pointi nne mfululizo na kuongoza 4-2. Svitolina alipata sare ya 6-6, lakini Zheng akafunga pointi ya ushindi katika mzunguko wake wa pili kwa seti 8-6.
"Alifanya vema katika seti ya pili. Pointi ile ya kuamua mshindi baada ya sare ilikuwa karibu sana. Sote wawili tumecheza kwa kiwango cha juu sana. Kusema kweli, nilitaka sana kushinda mechi hii, kwa hivyo nilihisi tashiwishi wakati nilipokuwa nikipiga mipira," Zheng amesema.
Zheng, ambaye alitumia siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 24 siku ya Alhamisi, amesema, "Natumai katika umri huu wa miaka 24 ninaweza kuwa mkomavu zaidi, na kuwa mtulivu kukabiliana na kila pointi kwenye uwanja wa tenisi. Hayo ni matarajio yangu mwenyewe."
Matokeo hayo yanampeleka Zheng kwenye nusu fainali yake ya pili ya China Open, inayolingana na mafanikio yake bora zaidi kwenye mashindano hayo, na nusu fainali yake ya kwanza ya WTA 1000 mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




