Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2026
Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China
Picha hii iliyopigwa tarehe 14 Oktoba 2026 ikionesha wajenzi wakitandaza reli kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo katika Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Xinhua/Li Bo)

Utandazaji wa reli umeanza rasmi jana Jumatano kwenye reli ya mwendo-kasi inayounganisha Mji wa Nantong wa Mkoa wa Jiangsu mashariki mwa China na Mji wa Ningbo wa Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China.

Mradi huo ni sehemu muhimu ya mtandao wa treni za mwendo-kasi wa China katika maeneo ya pwani, ambao unahusisha njia nane za reli za kutoka kaskazini na kuelekea kusini, na njia nane za reli za kutoka mashariki na kuelekea magharibi. Baada ya kukamilika kwake, njia mpya itasukuma mbele maendeleo jumuishi yenye sifa bora ya eneo la Delta ya Mto Changajing.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha