Karamu ya meza ndefu yafanyika Lanxi, mkoani Zhejiang, China, kuadhimisha Siku ya Chongyang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2026
Karamu ya meza ndefu yafanyika Lanxi, mkoani Zhejiang, China, kuadhimisha Siku ya Chongyang

Karamu ya meza ndefu, iliyoandaaliwa kwa ufadhili wa watu wenye ukarimu imefanyika jana Alhamisi katika Kijiji cha Yanggang, huko Lanxi, mkoani Zhejiang, Mashariki mwa China, ambapo watu zaidi ya 500 wenye umri wa miaka 60 na umri mkubwa zaidi wamealikwa kwenye karamu hiyo ya kuadhimisha Siku ya Chongyang ambayo ni siku ya wazee.

Siku hiyo ya Chongyang inaadhimishwa Tarehe 9 ya Mwezi wa 9 kila mwaka kwa kalenda ya kilimo ya China, ni fursa ya kuwajali na kuwatakia heri na baraka wazee nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha