Lugha Nyingine
Kundi la kwanza la vitu vya kuoneshwa kwenye Maonesho ya 9 ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) lawasili Shanghai (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2026
Kundi la kwanza la vitu vya kuoneshwa kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) limewasili mjini Shanghai, mashariki mwa China. Kundi hilo linajumuisha vifaa vya kiteknolojia, vifaa tiba, na bidhaa za kilimo na chakula; ambavyo baadhi yake vitaoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho hayo.
Kwa sasa maandalizi ya Maonesho hayo ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yanaendelea kwa bidii zote. Maonesho hayo yamepangwa kufanyika kwenye Kituo cha Kitaifa cha Maonesho na Mikutano (Shanghai) kuanzia tarehe 5 Novemba hadi 10 Novemba mjini Shanghai.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




