Katika picha: Eneo la viwanda vya sayansi na teknolojia vya kilimo katika Mji wa Jinhua mkoani Zhejiang, China (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2026
Katika picha: Eneo la viwanda vya sayansi na teknolojia vya kilimo katika Mji wa Jinhua mkoani Zhejiang, China
Mfanyakazi akikagua ndani ya banda la kilimo cha kisasa cha kijani kwenye eneo la viwanda vya sayansi na teknolojia ya kilimo katika Eneo la Jindong la Mji wa Jinhua mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, Oktoba 27, 2026. (Xinhua/Xu Yu)

Eneo la viwanda vya sayansi na teknolojia vya kilimo huko Jindong katika Mji wa Jinhua mkoani Zhejiang, mashariki mwa China lilianzishwa Septemba 2023, ni mradi wa vielelezo vya kilimo cha kisasa katika Jindong.

Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 13.2 hivi linahusisha mabanda ya kilimo cha kisasa cha kijani, mashamba yanayopangwa kwa vigezo maalum vya upandaji, pamoja na miundombinu mingine yanayounga mkono, kama vile vyanzo vya maji na sehemu ya maegesho ya magari.

Linalenga kujenga eneo la viwanda vya shughuli za jumla za kilimo cha kisasa linalofungamanisha utafiti na maendeleo ya miche, upandaji mimea ya ikolojia, utengenezaji wa kina wa mazao ya kilimo, uuzaji chapa, utalii, na vielelezo vya teknolojia ya kilimo. Katika eneo hilo kimeanzishwa kwa kilimo cha aina maalum za matunda na mboga za majani kama vile nanasi, matunda ya dragoni, na bluberi, pamoja na mboga ili kujenga mfano wa vielelezo katika uzalishaji wa matunda na mboga za majani za kitropiki za daraja la juu. Hatua hii imefufua rasilimali za ardhi ambazo hazikuwa zikitumika katika eneo hilo, na kuboresha muundo wa viwanda vya kilimo katika mkoa huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha