Banda la China lawa kivutio kwenye maonesho makubwa ya mambo ya filamu na televisheni barani Afrika (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2026
Banda la China lawa kivutio kwenye maonesho makubwa ya mambo ya filamu na televisheni barani Afrika
Picha iliyopigwa Oktoba 28, 2026 ikionesha Banda la China katika MIP Afrika 2026 jijini Cape Town, Afrika Kusini. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

CAPE TOWN - Banda la China limekuwa kivutio kwenye MIP Afrika 2026, shughuli kubwa ya mambo ya filamu na televisheni barani Afrika, likionesha aina mbalimbali za maudhui ya sauti na picha ya China, hali ambayo imekuza ubadilishanaji wa utamaduni na ushirikiano wa kitasnia kati ya China na bara la Afrika.

Banda hiyo la China linalofadhiliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China pamoja na Mamlaka ya Kitaifa ya Redio na Televisheni ya China, na kuandaliwa na Shirika la Utangazaji la Jiangsu, liliwaleta pamoja wawakilishi kutoka mashirika 16 ya China yanayojihusisha na sekta ya filamu na televisheni, ikiwemo utangazaji, utengenezaji wa filamu na televisheni, mambo ya katuni, na vyombo vya habari vya kitamaduni.

Waoneshaji ndani ya banda hilo walionesha kazi zaidi ya 50 za sauti na picha za China katika aina mbalimbali, zikiwemo tamthilia za televisheni, filamu za makala, vipindi mbalimbali vya burudani, na katuni, vilevile teknolojia za kisasa zaidi katika nyanja hiyo.

Wang Xiao, Kaimu Konsuli Mkuu wa China jijini Cape Town, ameliambia shirika la habari la China, Xinhua kuwa kazi za filamu na televisheni za China zimezidi kuwafikia watazamaji wa Afrika katika miaka ya hivi karibuni, hasa vijana, kutokana na ubadilishanaji wa kitamaduni na ya kati ya watu wa China na Afrika kuendelea kushamiri.

"Kazi bora za filamu na televisheni huwa kama dirisha na pia kifungo, zikijenga hali ya kuelewana na uhusiano wa karibu kati ya watu wa China na Afrika," amesema Wang. "Zinawezesha marafiki wa Afrika kufahamu zaidi kuhusu China, wakati huohuo zinasaidia watazamaji wa China kupata uelewa mzuri zaidi kuhusu Afrika."

Carol Weaving, Mkurugenzi Mtendaji wa RX Afrika—waandaaji wa MIP Afrika—amesema kuwa maudhui ya sauti na picha ya China yanaleta utajiri wa uelezaji simulizi, utaalamu wa uzalishaji maudhui, na uvumbuzi kwenye soko la Afrika, yakijumuisha tamthilia, katuni, filamu za makala, na miundo mipya ya kidijitali.

"Fursa ipo katika kubaini simulizi ambazo zinaendana na watazamaji wa Afrika, kuzifanya zipatikane kwa lugha inayofaa, kuzirekebisha kulingana na muktadha wa mahali husika na kuzisambaza, pamoja na kujenga uelewa wa kina zaidi kuhusu kile ambacho watazamaji kote barani mwetu wanataka," amesema Weaving.

MIP Afrika 2026 ilianza tarehe 28 na itafikia tamati leo tarehe 30 Oktoba kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Cape Town nchini Afrika Kusini, na imerekodi kampuni za kimataifa za vyombo vya habari zaidi ya 100 na washiriki zaidi ya 1,500. Imekuwa na ushiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Afrika Kusini, Nigeria, Kenya na Ghana. Kaulimbiu yake ni "Afrika. Isiyosimuliwa. Isiyozuilika. (Africa. Untold. Unstoppable.)" 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha