Lugha Nyingine
Njia ya kwanza kwenye anga ya chini ya kupeleka oda kwa droni kwenye kampasi za vyuo yazinduliwa mkoani Guizhou, China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 02, 2026
Hivi karibuni, mkoa wa Guizhou wenye sehemu nyingi za milimani, kusini magharibi mwa China umeanzisha rasmi njia yake ya kwanza kwenye anga ya chini ya kupeleka oda za wateja kwa droni kwenye maeneo ya kampasi za vyuo katika mji wa elimu ya ufundi stadi wa Qingzhen.
Njia hiyo ya usafirishaji kwenye anga ya chini inaunganisha maeneo ya biashara moja kwa moja na kampasi za vyuo, hivyo kupunguza muda wa kufikisha oda kwa walimu na wanafunzi hadi chini ya dakika 20, huku gharama za kuwasilisha oda zikianzia yuan 3.8 (dola takriban 0.57 za Marekani).
Huduma hii pia inasaidia kujenga jukwaa la mafunzo ambalo linafungamanisha shughuli za anga ya chini na elimu, ili kuunga mkono kazi ya kuwaandaa watu wenye ujuzi husika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




