Kundi la kwanza la mabehewa bapa ya kubeba kontena kwa ajili ya mradi wa ufufukaji wa TAZARA lakabidhiwa Dalian, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2026
Kundi la kwanza la mabehewa bapa ya kubeba kontena kwa ajili ya mradi wa ufufukaji wa TAZARA lakabidhiwa Dalian, China
Mfanyakazi akifanya kazi kwenye kituo cha Dalian cha kampuni ya CRRC Qiqihar Rolling Stock huko Dalian mkoani Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China, Novemba 24, 2026. (Xinhua/Pan Yulong)

Kundi la kwanza la mabehewa bapa 300 ya kubeba kontena kwa ajili ya mradi wa ufufukaji wa Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) limekabidhiwa huko Dalian mkoani Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China Jumanne wiki hii.

Mabehewa hayo yatasafirishwa kwa meli ya mizigo kutoka kituo cha Dalian cha kampuni ya CRRC Qiqihar Rolling Stock kwenda Tanzania na Zambia ili kuunga mkono uendeshaji wa njia nzima ya reli ya TAZARA na kuhakikisha huduma zake za ratiba ya kawaida.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha