Mkutano na waandishi wa Habari wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China unafanyika hapa Beijing.
Guo Weimin, msemaji wa mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, akishiriki kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing, China Tarehe 3, Machi. (Picha/Xinhua) Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limehimiza ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu katika nchi zinazoshiriki, alisema msemaji wa CCPPC Ijumaa wiki iliyopita.
BEIJING - China inalenga kufikia ukuaji wenye kasi wa uchumi wa karibu asilimia 5 na maendeleo yenye ubora wa juu Mwaka 2023, wakati nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani ikikusanya nguvu ili kufuata mwelekeo wa ufufukaji wa uchumi na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa. Lengo hilo la ukuaji wa uchumi lililowekwa, ambalo ni la juu zaidi ya ukuaji wa asilimia 3 uliorekodiwa katika Pato la Taifa (GDP) mwaka jana, ni moja ya malengo muhimu ya maendeleo yaliyoainishwa kwenye ripoti ya kazi ya serikali iliyotolewa na Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang kwa Buge la Umma la 14 la China, ambalo limeanza mkutano wake wa kila mwaka jana Jumapili.