人民网首页

Habari

Kiongozi Mwandamizi wa CPC ashiriki kwenye majadiliano ya ujumbe wa Taiwan kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la 14 la China

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Taiwan kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) unaofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 9, 2023. (Xinhua/Liu Bin) BEIJING - Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Alhamisi alishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Taiwan kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC).

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kuchagua viongozi wapya

Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akiongoza kikao cha tatu cha Tume Tendaji ya Wenyeviti ya mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPCCC) kilichofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 9, 2023. (Xinhua/Shen Hong) BEIJING - Orodha ya wagombea wa uongozi mpya wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), ambacho ni chombo kikuu cha ushauri wa kisiasa cha China, imeidhinishwa Alhamisi.

Mpango wa Mageuzi ya Vyombo vya Baraza la Serikali la China wapitishwa

Kikao cha tatu cha mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China kikifanika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma tarehe 10, Machi, 2023. (PIcha inatoka Xinhua) Tarehe 10, Machi, Bunge la Umma la China limepitisha mpango wa mageuzi ya vyombo vya baraza la serikali la China.

Mageuzi ya vyombo vya Baraza la Serikali la China ni hatua muhimu ya kutawala nchi kwa njia ya kisasa

Mageuzi ya vyombo vya baraza la serikali la China ni hatua muhimu ya kuongeza uwezo wa utawala na kuinua ufanisi katika mazingira ya dunia yenye utatanishi, na inalenga kukamilisha majukumu mapya ya kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa Mpango wa mageuzi ya vyombo vya baraza la serikali la China unaofikishwa ili kuthibitishwa kwenye mkutano wa Bunge la Umma la 14 la China unaweka mkazo katika kuondoa matatizo magumu yanayofuatiliwa na watu , na yataleta ushawishi mkubwa kwa maendeleo ya jamii na uchumi ya China. Mageuzi hayo yanasisitiza sekta mbalimbali muhimu za ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, kama vile sayansi na teknolojia, usimamizi wa mambo ya fedha, usimamizi wa data, ustawishaji wa vijiji, hakimiliki ya ubunifu na huduma za utunzaji wa wazee.

Iliyopita1 2 3 4 5 6 Inayofuata