人民网首页

Habari

Matokeo ya uchunguzi kuhusu Mikutano Miwili 2023 ya China yaonesha watu wanafuatilia zaidi masuala ya elimu na vipaji, huduma za jamii na kupambana na ufisadi

Kuanzia tarehe 1 hadi 27, Februari, tovuti ya Gazeti la Umma ilifanya uchunguzi kuhusu mikutano miwili 2023 ya China, yaani mkutano wa Bunge la Umma la China na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China. Uchunguzi huo ni wa 22 kufanywa na tovuti hiyo, na umevutia watu zaidi ya milioni 5.

Wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China wakitia saini ya kujiandikisha kwenye mahudhurio, kuchukua vitamubulisho na nyaraka za mkutano kwenye Kituo cha Mikutano cha Beijing Tarehe 2, Machi. (Picha na mwandishi wa habari wa tovuti ya Gazeti la Umma, Wang Tianle)

Wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China watia saini ya kujiandikisha kwenye mahudhurio

Mikutano mikuu miwili ya Mwaka 2023 ya China, yaani Mkutano wa Bunge la Umma la China na Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China inawadia. Tarehe 2, wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China kutoka baadhi ya makundi wametia saini ya kujiandikisha kwenye mahudhurio kwa utaratibu chini ya uongozi wa wahudumu, na kujitayarisha kuhudhuria kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China utakaofunguliwa Tarehe 4, Machi.

Mkutano na Waandishi wa Habari wa Mkutano wa Kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China kufanyika Tarehe 3, Machi

Mkutano na Waandishi wa Habari wa Mkutano wa Kwanza wa Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China utafanyika leo saa 10:30 Jioni Tarehe 3, Machi Ijumaa (kwa saa za Beijing) kwenye ukumbi wa habari ulioko ghorofa ya kwanza ya Jumba la Mikutano ya Umma, ambapo msemaji wa mkutano huo Guo Weimin atajulisha hali ya mkutano huo kwa waandishi wa habari wa China na wa nchi mbalimbali na kujibu maswali yao. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na tovuti ya Xinhua zitatangaza moja kwa moja hali ya mkutano huo.

Mkutano na Waandishi wa Habari wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China kufanyika Tarehe 4, Machi

Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China utafanya mkutano na waandishi wa habari Jumamosi saa 6 mchana (kwa saa za Beijing) Tarehe 4, Machi kwenye ukumbi wa habari wa Jumba la Mikutano ya Umma, ambapo msemaji wa mkutano huo atajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari wa China na wa nchi mbalimbali kuhusu ajenda ya mkutano huo na kazi za Bunge la Umma la China. Siku hiyo Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) litatangaza moja kwa moja hali ya mkutano huo, huku tovuti ya China itatangaza moja kwa moja kwa kupitia picha na maandishi.

Iliyopita6 7 8 9 10 11 Inayofuata