BEIJING - Wajumbe na washauri wa kisiasa wa Kitaifa wenye asili ya Taiwan wametoa utambuzi wao wa sehemu zinazohusu Taiwan katika ripoti ya kazi ya serikali ya China na kupaza sauti ya upingaji wao thabiti kwa shughuli za "Kujitenga kwa Taiwan" na uingiliaji wa nje. Ripoti hiyo inajadiliwa katika mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China, au bunge kuu la China.
BEIJING - Viongozi waandamizi wa China Ijumaa walihudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, unaoendelea mjini Beijing, mji mkuu wa China. Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, Wang Huning ameshiriki katika kikao cha majadiliano cha kundi la wajumbe wa Bunge hilo kutoka Taiwan.
Kikao cha pili cha wajumbe wote cha Mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) kimefanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Ijumaa, Machi 7.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 2025, 2027. (Xinhua/Li Genge) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Ijumaa alipokuwa akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, unaoendelea mjini Beijing, mji mkuu wa China, amesisitiza kuhitimisha kwa mafanikio Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya jeshi (2021-2025).