BEIJING - China imeweka lengo la ukuaji uchumi la karibu asilimia 5 kwa mwaka 2025, ikionyesha mtazamo mzuri wa kiuchumi licha ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika duniani, kwani watunga sera wa nchi hiyo wamedhamiria kuhakikisha uchumi unaimarika kwa utulivu kupitia hatua madhubuti yenye ufanisi. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Li Qiang Jumatano alitangaza lengo hilo wakati akitangaza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China unaondelea mjini Beijing kwa ajili ya kujadiliwa.
(Ding Haitao/Xinhua) Mkutano wa Tatu wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) umefunguliwa leo Jumatano kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, ambapo wajumbe takriban 3000 kutoka maeneo, makabila na sekta mbalimbali kote nchini humo wanahudhuria. Wakati wa mkutano huo wa wiki moja, wajumbe watasikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali, kuhitimisha matokeo ya kazi yaliyopatikana katika mwaka uliopita na kuweka mipango kuhusu maendeleo ya nchi hiyo katika mwaka mpya.
BEIJING – Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambacho ni chombo kikuu cha mashauriano ya kisiasa cha China, imefanya mkutano wake wa mwaka Jumanne, Machi 4 mjini Beijing, China. Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine walihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa tatu cha Kamati hiyo ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC, uliofunguliwa saa 9 alasiri (kwa saa za Beijing) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China Katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen) BEIJING – Wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China wamekusanyika mjini Beijing siku ya Jumanne kwenye kikao cha matayarisho cha mkutano wa tatu wa bunge hilo la 14 la China utakaoanza leo Jumatano, ili kuchagua Tume Tendaji wa mkutano na kupanga ajenda zake.