Mawaziri wa China, Lu Zhiyuan wa Wizara ya Mambo ya Kiraia, Wang Xiaoping wa Wizara ya Rasilimali Watu na Hifadhi ya Jamii, Ni Hong wa Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji-Vijiji, na Lei Haichao Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Afya ya China wamehudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumapili wakifafanua na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu maisha ya watu kwenye mkutano na waandishi wa habari katika wakati wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China unaondelea mjini Beijing.
Jana Jumamosi, Machi 8 ilikuwa Siku ya Wanawake Duniani na katika mikutano mikuu miwili ya mwaka ya Bunge la Umma la China na ule wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, wajumbe na washauri wa kisiasa wanawake wana jukumu muhimu katika kuunganisha hekima ili kuhimiza maendeleo ya nchi hiyo.
Mawaziri wa Serikali ya China wamehudhuria mahojiano na waandishi wa habari na kujibu maswali mbalimbali kuhusu masuala ya wizara wanazoziongoza jana Jumamosi, Machi 8, baada ya kikao cha pili cha wajumbe wote cha mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China unaondelea kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China.
Kikao cha pili cha wajumbe wote cha Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China unaoendelea kimefanyika mjini Beijing, mji mkuu wa China jana Jumamosi, Machi 8.