Liu Jieyi, msemaji wa Mkutano wa Tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 3, 2025. (Xinhua/Li He) BEIJING - Msemaji wa Mkutano wa Tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, ambalo ni chombo kikuu cha mashauri ya kisiasa cha China, Liu Jieyi, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatatu kwamba hali ya msingi na mwelekeo wa kimsingi wa maendeleo mazuri ya muda mrefu ya uchumi wa China bado haujabadilika.
BEIJING - Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambalo ni chombo kikuu cha kutoa mashauri ya kisiasa cha China utafanya mkutano wake wa mwaka kuanzia leo Jumanne, Machi 4 hadi 10 mjini Beijing, msemaji wa mkutano huo amesema jana Jumatatu. “Mkutano huo wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC umepangwa kuanza leo Jumanne saa 9 mchana (kwa saa za Beijing) na kufungwa asubuhi ya Machi 10,” msemaji Liu Jieyi amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akiongoza na kutoa hotuba kwenye mkutano wa 10 wa Kamati ya wajumbe wa kudumu ya Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC uliofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 2. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING - Kamati ya 14 ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambayo ni chombo cha kitaifa cha China cha mashauriao ya kisiasa, imemaliza mkutano wa kumi wa kamati yake ya wajumbe wa kudumu mjini Beijing jana Jumapili.
BEIJING – Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amewataka maofisa waandamizi wa chama kubeba wajibu mpya na kuchukua hatua mpya kwa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China. Xi amesema hayo baada ya kusoma ripoti za kazi za mwaka za viongozi waandamizi wa Chama zilizowasilishwa hivi karibuni kwa Kamati Kuu ya Chama na Katibu Mkuu wake.