(Mpiga picha:Liu Dawei/Xinhua) BEIJING - China itatoa uhakika kwa dunia hii isiyo na uhakika, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Wang ameuambia mkutano na waandishi wa habari mapema leo Ijumaa pembezoni mwa mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la China unaoendelea mjini Beijing. "Tunaishi kwenye dunia inayobadilika na yenye misukosuko, ambapo uhakika unazidi kuwa rasilimali adimu," amesema "Diplomasia ya China itasimama bila kuyumba kwenye upande sahihi wa historia na upande wa upigaji hatua wa binadamu.
BEIJING - Viongozi waandamizi wa China Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi Alhamisi walihudhuria vikao vya majadiliano katika mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China na vikundi vya majadiliano kwenye mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC). Waziri mkuu Li Qiang alishiriki kwenye majadiliano ya kikundi cha wajumbe wa Mkoa wa Hebei wanaohudhuria Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la umma, ambapo amehimiza mkoa huo kutumia fursa ya kufanya ushirikiano na uratibu katika maendeleo ya Beijing-Tianjin-Hebei ili kujipatia maendeleo zaidi.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka vyama vya kidemokrasia vya China vya Shirikisho la Demokrasia la China na Shirikisho la Uhimizaji wa Demokrasia la China, na sekta ya elimu, ambao wanahudhuria mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China mjini Beijing, Machi 6, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza kuimarisha umuhimu wa elimu katika kuunga mkono maendeleo ya sayansi na teknolojia na kuandaa vipaji, akitoa wito wa kuelewa kwa kina mahitaji ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China kwa elimu, sayansi na teknolojia, na vipaji.
Wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China jana Jumtano alasiri wamefanya vikao vya kujadili ripoti ya kazi ya serikali aliyotoa Waziri Mkuu wa China Li Qiang kwenye mkutano huo unaofanyika Beijing.