Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akiwatembelea wajumbe wa waandishi wa habari walioripoti habari za mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi) BEIJING - Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) amewatembelea wajumbe wa waandishi wa habari walioripoti habari za mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC uliomaizika jana Jumatatu mjini Beijing.
(Picha/Xinhua) Kikao cha tatu cha Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) kimefungwa leo hapa Beijing baada ya kukamilisha ajenda mbalimbali. Mkutano wa ufungaji wa kikao kicho umepitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya baraza hilo, azimio kuhusu ripoti ya kazi ya ushughulikiaji wa mapendekezo tangu kikao cha pili cha baraza hilo, ripoti ya uchunguzi wa mapendekezo ya kikao kicho iliyowasilishwa na kamati inayoshughulikia mapendekezo ya baraza hilo, na azimio la kisiasa la kikao hicho.
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye ofisi ya sekretarieti ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 9, 2025. (Xinhua/Zheng Huansong) BEIJING – Watunga sheria wa kitaifa wa China wamewasilisha mapendekezo 269 hadi Machi 8 ambayo ni tarehe ya mwisho kuwasilisha mapendekezo kwa mkutano mkuu wa tatu unaoendelea mjini Beijing wa Bunge la Umma la 14 la China, ambao ni mkutano wa mwaka wa chombo hicho kikuu cha utungaji wa sheria.
BEIJING - Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambacho ni chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, jana Jumapili ilifanya kikao cha tatu cha wajumbe wote cha mkutano mkuu wa mwaka unaoendelea mjini Beijing, na Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China , alihudhuria kikao hicho. Kwenye kikao hicho, washauri wa kisiasa wa kitaifa 14 wametoa maoni yao kuhusu mada mbalimbali ambapo maofisa waandamizi kutoka Kamati Kuu ya CPC na Baraza la Serikali la China walialikwa kusikiliza mapendekezo .