Akiwa amekabidhiwa kazi na Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, Li Hongzhong, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano akiongoza kikao cha tatu cha tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei) BEIJING – Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, ambalo ni chombo cha utungaji wa sheria cha kitaifa cha China, imefanya kikao chake cha tatu jana Jumatatu, ambapo akiwa amekaimishwa kazi na Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano Li Hongzhong ameongoza kikao hicho.
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye ofisi ya sekretarieti ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 9, 2025. (Xinhua/Zheng Huansong) BEIJING – Watunga sheria wa kitaifa wa China wamewasilisha mapendekezo 269 hadi Machi 8 ambayo ni tarehe ya mwisho kuwasilisha mapendekezo kwa mkutano mkuu wa tatu unaoendelea mjini Beijing wa Bunge la Umma la 14 la China, ambao ni mkutano wa mwaka wa chombo hicho kikuu cha utungaji wa sheria.
Mawaziri wa China, Lu Zhiyuan wa Wizara ya Mambo ya Kiraia, Wang Xiaoping wa Wizara ya Rasilimali Watu na Hifadhi ya Jamii, Ni Hong wa Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji-Vijiji, na Lei Haichao Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Afya ya China wamehudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumapili wakifafanua na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu maisha ya watu kwenye mkutano na waandishi wa habari katika wakati wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China unaondelea mjini Beijing.
Feng Xingya, mwenyekiti wa kundi la kampuni za kuunda magari la China, GAC, amekuwa akifanya kazi katika tasnia ya magari kwa miaka zaidi ya 30. Ameshuhudia maendeleo ya tasnia ya magari ya China.