Mkutano wa COP15 wafunguliwa Kunming, China ukiwa na kaulimbiu juu ya ustaarabu wa kiikolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2021
Mkutano wa COP15 wafunguliwa Kunming,  China ukiwa na kaulimbiu juu ya ustaarabu wa kiikolojia
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2021 ikionesha ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa nchi zinazosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Baiolojia Anuai (COP15) huko Kunming, Mji Mkuu wa Mkoa wa Yunnan uliopo Kusini Magharibi mwa China. (Xinhua / Li Xin)

KUNMING, Oktoba 11 (Xinhua) - Mkutano wa 15 wa nchi zinazosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu Baiolojia Anuai unaojulikana kama COP15, umeanza rasmi Jumatatu alasiri huko Kunming, Mji Mkuu wa Mkoa wa Yunnan ulioko Kusini Magharibi mwa China.

Ukiwa na kaulimbiu ya "Ustaarabu wa Kiikolojia: Kujenga Hatma ya Pamoja ya Viumbe hai Duniani," COP15 ni mkutano wa kwanza wa dunia ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa ukionesha ustaarabu wa kiikolojia, ambao ni falsafa iliyopendekezwa na China.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza, iliyopangwa Oktoba 11 hadi 15, inafanyika kupitia njia mbili za mtandaoni na nje ya mtandao.

Sehemu ya pili ya mkutano huo, itakayofanyika ana kwa ana katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2022, inatarajiwa kufikia na kupitisha mpango kabambe wa viumbe anuai duniani baada ya Mwaka 2020.

China ni miongoni mwa nchi za kwanza zinazosaini Mkataba wa Baiolojia Anuai, ambao ulianza kutekelezwa Mwaka 1993. Mkataba huo sasa una watia saini wapatao 196, na Mkutano nchi zinazosaini mkataba huo ndio utaratibu wa juu zaidi wa kujadili na kufanya maamuzi kuhusu Mkataba huo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha