Sisi ni wanaojitolea! (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 11, 2022
Sisi ni wanaojitolea!
Katika kituo kimoja cha upimaji wa virusi vya korona cha makazi ya Beilang ya Mtaa wa Jianwai wa Eneo la Chaoyang, Bian Meng, mmoja wa wanaojitolea aliyetoka ofisi moja ya wanasheria ya Beijing akisaidia mtu wa kupimwa kujiandikisha kwa njia ya simu. (Picha ilipigwa Mei 9.) Bian Meng alizaliwa Mwaka 1999, na hii ni mara ya nne kwake kushiriki kwenye kazi ya ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona. Alisema kuwa mimi ni kijana, ninatakiwa kubeba jukumu na kutoa mchango wangu.

Katika siku za hivi karibuni, maambukizi ya virusi vya korona yametokea katika maeneo mengi mjini Beijing. Watu wengi walijituma kwenye kazi za ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona, wakishiriki kwenye kazi za upimaji wa virusi vya korona na nyinginezo. Miongoni mwao, kuna wafanyakazi wa makampuni, watu waliostaafu, na wanafunzi watakaohitimu kutoka vyuo vikuu waliozaliwa katika miaka ya 2000. Walifanya kazi kwa kadri wawezavyo na kutoa michango yao kwa ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona. (Mpiga picha: Ju Huanzong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha