Sisi ni wanaojitolea! (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 11, 2022
Sisi ni wanaojitolea!
Katika kituo kimoja cha upimaji wa virusi vya korona cha Mtaa wa Balizhuang wa Eneo la Chaoyang, Li Surong mwenye umri wa miaka 62,mmoja wa wanaojitolea ambaye amestaafu na pia ni mwanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China akiongoza watu walioshiriki kwenye upimaji wa virusi vya korona kujiandikisha kwa njia ya simu. (picha ilipigwa Mei 8.) Li Surong alijiunga na kazi ya kujitolea ya ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona katika kikundi cha Wechat, alisema kuwa watu wanahitajika kufanya kazi, kwahivyo niko hapa.

Katika siku za hivi karibuni, maambukizi ya virusi vya korona yametokea katika maeneo mengi mjini Beijing. Watu wengi walijituma kwenye kazi za ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona, wakishiriki kwenye kazi za upimaji wa virusi vya korona na nyinginezo. Miongoni mwao, kuna wafanyakazi wa makampuni, watu waliostaafu, na wanafunzi watakaohitimu kutoka vyuo vikuu waliozaliwa katika miaka ya 2000. Walifanya kazi kwa kadri wawezavyo na kutoa michango yao kwa ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona. (Mpiga picha: Ju Huanzong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha