Sisi ni wanaojitolea!

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 11, 2022
Sisi ni wanaojitolea!
Katika kituo kimoja cha upimaji wa virusi vya korona cha Mtaa wa Balizhuang wa Eneo la Chaoyang, Zhang Shuqi, mmoja wa wanaojitolea aliyetoka kampuni moja ya Media akiongoza watu walioshiriki kwenye upimaji wa virusi vya korona kujipanga foleni kwa utaratibu. (Picha ilipigwa Mei 8.) Zhang Shuqi ana umri wa miaka 25 mwaka huu , na hii ni mara ya kwanza kwake kushiriki kwenye kazi ya ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona.

Katika siku za hivi karibuni, maambukizi ya virusi vya korona yametokea katika maeneo mengi mjini Beijing. Watu wengi walijituma kwenye kazi za ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona, wakishiriki kwenye kazi za upimaji wa virusi vya korona na nyinginezo. Miongoni mwao, kuna wafanyakazi wa makampuni, watu waliostaafu, na wanafunzi watakaohitimu kutoka vyuo vikuu waliozaliwa katika miaka ya 2000. Walifanya kazi kwa kadri wawezavyo na kutoa michango yao kwa ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona. (Mpiga picha: Ju Huanzong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha