

Lugha Nyingine
Sisi ni wanaojitolea! (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 11, 2022
![]() |
Katika kituo kimoja cha upimaji wa virusi vya korona cha makazi ya Beilang ya Mtaa wa Jianwai wa Eneo la Chaoyang, Chen Qiyao, mmoja wa wanaojitolea aliyezaliwa katika miaka ya 2000, akisaidia watu walioshiriki kwenye upimaji wa virusi vya korona kujiandikisha kwa njia ya simu. (picha ilipigwa Mei 9.) Chen Qiyao alizaliwa Mwaka 2000 na atahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Pili cha Beijing, pia ni mwanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China, na hii ni mara ya tano kwake kushiriki kwenye kazi ya ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona. |
Katika siku za hivi karibuni, maambukizi ya virusi vya korona yametokea katika maeneo mengi mjini Beijing. Watu wengi walijituma kwenye kazi za ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona, wakishiriki kwenye kazi za upimaji wa virusi vya korona na nyinginezo. Miongoni mwao, kuna wafanyakazi wa makampuni, watu waliostaafu, na wanafunzi watakaohitimu kutoka vyuo vikuu waliozaliwa katika miaka ya 2000. Walifanya kazi kwa kadri wawezavyo na kutoa michango yao kwa ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona. (Mpiga picha: Ju Huanzong/Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma