Sehemu ya Reli ya Dali-Baoshan ya Reli ya Dali-Ruili nchini China kuanza kutumika
 |
Treni ya mwendokasi ikiendeshwa kwa majaribio kwenye daraja kuu la Mto Lancang katika sehemu ya reli ya Dali-Baoshan ya Reli ya Dali-Ruili katika Mkoa wa Yunnan nchini China, Julai 19, 2022. Sehemu ya reli ya Dali-Baoshan ya Reli ya Dali-Ruili itaanza kutumika hivi karibuni, na hivyo kumaliza hali ya kutounganishwa na mtandao wa reli kwa eneo la Baoshan. Ikiwa na urefu wa kilomita 330, Reli hiyo ya Dali-Ruili ni mradi mkubwa kwenye mpango wa ujenzi wa mtandao wa reli wa China. (Xinhua/Chen Xinbo) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)