Kampuni ya uchimbaji visima ya China yasaidia kugeuza jangwa la Misri kuwa shamba la kijani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2022
Kampuni ya uchimbaji visima ya China yasaidia kugeuza jangwa la Misri kuwa shamba la kijani
Mtambo wa kuvuna ukivuna viazisukari kwenye shamba lililoko jangwani katika Mkoa wa Minya, Misri Julai 11, 2022. (Xinhua/Sui Xiankai)

MINYA – Huku mtambo mkubwa wa kuvuna viazisukari ukipitia shamba kubwa katika jangwa Magharibi mwa Mkoa wa Minya Kusini mwa Misri, malori mengi yalikuwa yakipakia viazisukari vilivyovunwa na kuvisafirisha hadi kiwanda cha kusindika umbali wa kilomika 40 kwa barabara.

"Sasa tuna furaha kubwa na kiasi cha sukari tunachopata kutoka kwenye viazisukari. Huu utakuwa mwaka wetu wa pili na tumeona ongezeko la asilimia 50 la mavuno zaidi ya mwaka jana, kwa hivyo tunahisi kwamba tumefanikiwa. tumepata modeli nzuri sana na tunaweza kutengeneza mazao ambayo yanaweza kukipa malighafi kiwanda," anasema Aaron Baldwin, meneja mkuu wa kilimo wa Kampuni ya Canal Sugar, ambayo ni ya ubia wenye thmani ya dola bilioni 1 za Kimarekani kati ya Misri na Falme za Kiarabu (UAE).

Mradi wa Sukari ya Canal unalenga kugeuza hekta 50,000 za jangwa kuwa shamba la kilimo ili kukidhi mahitaji makubwa ya viazisukari kwa kiwanda hicho. Ili kufanya hivyo, ni muhimu kupata maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliaji.

"Tulifika katikati ya jangwa na kwa msaada wa kampuni ya China ya Zhongman Petroleum and Natural Gas (ZPEC), tulianza kufanya uchunguzi wa visima, kisha tukatengeneza mtandao unaotuwezesha kuanza kumwagilia maji." Baldwin ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, na kuongeza kuwa "mradi huo utakapokamilika, kutakuwa na visima takriban visima 330 hadi 350 vilivyojaa maji."

Huku zaidi ya visima 150 vya maji vikiwa vimechimbwa, mashamba makubwa ya viazisukari yametawanyika katika jangwa, na kutengeneza shamba kubwa la kutoa malighafi kwa kiwanda cha kusindika viazisukari.

"Mahali hapa palikuwa jangwa tu tulipoanzisha mradi huu Mwaka 2018, lakini sasa pamegeuka kuwa shamba la umwagiliaji na visima tulivyochimba na kupanda viazivitamu, alfalfa na shayiri, ambayo inatufanya tujisikie fahari," anasema Zhou Guiqiang, msukuma zana wa ZPEC, tawi la Misri.

Kwa upande wake, Ahmed Soliman, meneja wa msingi wa ZPEC, amesema kuwa alijiunga na kampuni hiyo ya China Mwaka 2019 na alijiunga na mradi wa Sukari ya Canal mapema Mwaka 2020.

"Ninajisikia furaha kushiriki katika kugeuza jangwa hili kuwa la kijani. Ni kama ndoto. Nilipokuja hapa kwa mara ya kwanza, sikufikiria kwamba siku moja litageuzwa kuwa shamba hili kubwa," Ahmed ameliambia Xinhua.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha