Maji machafu yaliyochafuliwa kwa mionzi ya nyuklia ya Japani yachochea hasira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2023

Maandamano sehemu yametokea katika nchi mbalimbali baada ya Japan kutiririsha maji machafu yenye mionzi ya nyuklia kwenye Bahari ya Pasifiki kutoka kwenye kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi kilichoharibika.

Waandamanaji wa Korea Kusini wakiingia mitaani mjini Seoul siku ya Jumamosi baada ya hatua ya Japan ya kutiririsha baharini maji machafu yenye mionzi ya nyuklia kutoka kinu cha nyuklia cha Fukushima Daiichi kilichoharibika. (LEE JIN-MAN/AP)

"Japan, nina hasira!" "Iweke Bahari yetu ya Pasifiki isiyokuwa na nyuklia!"

Tarehe 25 Agosti, mamia ya raia wa nchi ya visiwa ya Fiji waliandamana kwenye mitaa katika mji mkuu wao, Suva, wakipaza sauti zao kwa nguvu dhidi ya Japan kutiririsha maji yenye sumu ya nyuklia kwenye Bahari ya Pasifiki.

Waandamanaji, wakiongozwa na Muungano wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Haki za Binadamu ya Fiji, wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za kimataifa kusitisha hatua hiyo ya Tokyo na kulinda bahari na vizazi vijavyo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha