China yaitaka Marekani kuacha kutia sumu katika uungaji mkono wa umma kwa uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2024

BEIJING - China inaitaka Marekani kuacha kutia sumu uungaji mkono wa umma kwa uhusiano wa pande mbili, na kurekebisha makosa yake ya kuwanyanyasa, kuwahoji na kuwafukuza raia wa China bila sababu yoyote, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesema Jumatano.

Hivi majuzi gazeti la Washington Post lilichapisha ripoti maalum kuhusu mahojiano na wanafunzi sita na wasomi wawili wa vyuo wa China ambao walinyanyaswa, kuhojiwa, na kufukuzwa nchini humo bila sababu yoyote wakati wa kuingia Marekani. Ripoti hiyo ilitoa maelezo juu ya kile kilichowapata baadhi yao na ilifuatiliwa sana nchini Marekani.

Katika kujibu swali husika, Lin amesema China imerudia mara kwa mara msimamo wake wa kupinga Marekani kuwanyanyasa, kuwahoji na kuwafukuza raia wa China, hasa wanafunzi na wasomi bila sababu yoyote.

Marekani mara kwa mara inatumia usimamizi wa utekelezaji wa sheria ulio wa kibaguzi, wa kisiasa na wa kulenga watu dhidi ya wanafunzi wa China, ambao unakiuka kwa kiasi kikubwa haki halali na maslahi ya watu wanaohusika, kuvuruga usafiri wa kawaida wa kuvuka mpaka kati ya China na Marekani, ni kinyume na dhamira ya Marekani ya kuwezesha na kuunga mkono mawasiliano ya kitamaduni na ya kati ya watu kati ya nchi hizo mbili na inakiuka matakwa ya pamoja ya watu wa pande hizo mbili katika kufanya mawasiliano ya kirafiki, Lin amesema.

"Tunaitaka Marekani isikilize kwa dhati sauti za watu wa sekta mbalimbali za nchi hizo mbili, kuacha kutia sumu uungaji mkono wa umma kwa uhusiano wa pande mbili, kurekebisha makosa yake ya kuwanyanyasa, kuwahoji na kuwafukuza raia wa China bila sababu, na kuchunguza kwa kina kesi husika ili kutoa maelezo kwa waathiriwa," Lin amesema.

Amesema China itaendelea kuchukua hatua madhubuti kulinda haki halali na maslahi ya raia wa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha