Watu wawili wafariki kwenye ajali ya barabarani mashariki mwa Tanzania

(CRI Online) Machi 29, 2024

Watu wawili wamefariki na wengine watano wamejeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana na lori la mafuta, na kusababisha moto katika mkoa wa Pwani mashariki wa Tanzania.

Watu wawili wamefariki na wengine watano wamejeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana na lori la mafuta, na kusababisha moto katika mkoa wa Pwani mashariki wa Tanzania.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri kwa saa za huko, kufuatia mabasi yaliyokuwa yakielekea mikoa ya kusini kugongana na lori la mafuta katika upande mwingine wa barabara yalipojaribu kupita magari mengine kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam-Morogoro.

Ofisa huyu amesema, abiria wote, licha ya wawili waliofariki na watatu waliojeruhiwa, walifanikiwa kutoka kwenye mabasi yao kabla ya kuwaka moto.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha