Rais wa zamani wa Afrika Kusini Zuma azuiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2024

(CRI Online) Machi 29, 2024

Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC) imesema imedumisha pingamizi lililowekwa dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi ujao.

Mwenyekiti wa IEC Mosotho Moepya amesema katika mkutano wa waandishi wa habari kwamba wamepokea pingamizi 82 kuhusu wagombea waliopendekezwa na vyama 21 vya siasa kwa ajili ya uchaguzi wa kitaifa na majimbo wa mwaka 2024, likiwemo pingamizi dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma, ambalo wamelikubali.

Afrika Kusini itafanya uchaguzi wa kitaifa na serikali za mitaa tarehe 29 mwezi Mei.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha