WHO yatoa zana za mkononi kwa ajili ya kuboresha uhifadhi data za utoaji chanjo nchini Kenya

(CRI Online) Machi 29, 2024

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Abdourahmane Diallo, amesema shirika hilo limetoa vifaa 940 vinavyohama ili vitumike kuweka kidijitali michakato ya chanjo nchini Kenya.

Bw. Diallo amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi, kuwa vifaa hivyo vikiwa ni pamoja na kompyuta za mkononi, vitasaidia kuwezesha watoa chanjo kuboresha sifa na uthibitisho wa data za chanjo nchini Kenya. Amesema vifaa hivyo vitachukua nafasi ya hati za karatasi kwa chanjo, na hivyo kupunguza makosa makubwa ya data. WHO pia imetoa nguo maalum kwa ajili ya wahudumu wa mwitikio wa haraka.

Waziri wa afya wa Kenya Bibi Susan Nakhumicha, ameutaja mchango huo kutoka WHO, kuwa ni chachu ya kazi ya Mpango wa taifa wa chanjo na kinga.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha