Watu wa sehemu mbalimbali nchini China wafurahia mila na jadi za Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2025
Watu wa sehemu mbalimbali nchini China wafurahia mila na jadi za Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Watalii wakifurahia maonyesho ya "maua ya chuma", ambayo ni maonyesho ya sanaa ya kijadi ya kurusha chuma kilichoyeyushwa ili kukifanya kionekane kama fashifashi, kwenye vyelezo vya mianzi kando ya Mto Gongshui katika Wilaya ya Xuanen, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Januari 22, 2025. (Picha na Song Wen/Xinhua)

Tarehe 29 Januari itakuwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China 2025, hali ya furaha ya kukaribisha sikukuu hiyo muhimu kwa Wachina inaonekana katika sehemu mbalimbali nchini China. Watu wa China wanafurahia mila na jadi za sikukuu hiyo na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za sikukuu hiyo. Kwa kalenda ya kilimo ya China, Tarehe 29 Januari itakuwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, na kuanzia siku hiyo utakuwa Mwaka wa Nyoka wa jadi wa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha