Kutoka ramani hadi undugu, uwanja wa AFCON wa Tanzania wainuka kwa uungaji mkono wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2025
Kutoka ramani hadi undugu, uwanja wa AFCON wa Tanzania wainuka kwa uungaji mkono wa China
Li Lin, meneja mtendaji wa mradi wa Kundi la Kampuni za Uhandisi wa Ujenzi wa Reli la China (CRCEG), akizungumza katika mahojiano mjini Arusha, Tanzania, Aprili 25, 2025. (Xinhua/Li Yahui)

DAR ES SALAAM - Mustafa Hashim Chikawe, mwenye umri wa miaka 35, mhandisi wa umeme na mitambo, alikuwa amesimama kwenye eneo lenye pilika nyingi za ujenzi wa uwanja wa michezo wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania. Macho yake yalikuwa yameelekezwa kwenye kreni ndefu za minara huku zikiinua nguzo za chuma angani.

Akiwa baba wa watoto watatu, Mustafa amekuwa akifanya kazi kwenye ujenzi huo kwa muda wa miezi tisa akiwa na Kundi la Kampuni za Uhandisi wa Ujenzi wa Reli la China (CRCEG), akisimamia ufungaji wa mifumo ya umeme na mabomba.

"Nilipata kazi hii kwa sababu nilimvutia bosi wangu katika mradi wa awali," Mustafa amesema, huku akionyesha majivuni kwa hisia ya sauti yake. Amekumbushia muda wake wa kufanya kazi na kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (East Africa), ambapo alishiriki kwenye ujenzi wa hoteli na majengo ya serikali.

"Kutokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi na kampuni za China, nimejifunza kuwa wanawasilisha kazi za hali ya juu na wanadhamiria sana," amesema.

Lakini kwa Mustafa, umuhimu wa uwanja huo unaenda mbali zaidi ya mradi rahisi.

Ukiwa umejengwa dhidi ya mwonekano wa ukungu wa Mlima Meru, muundombinu huo wa chuma unaoinuka unajumuisha ndoto, ambayo ni dira ya mageuzi kwa Arusha, jiji ambalo mara nyingi huitwa "Geneva ya Afrika" kwa kuwa mwenyeji wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na mashirika mengi ya kimataifa.

“Mara mradi huu utakapokamilika tutakuwa tumeboresha miundombinu kwa kiasi kikubwa, hasa ikizingatiwa kuwa Arusha ni mkoa wa kitalii,” amesema.

Simulizi kama hizo ni za kawaida katika eneo la ujenzi wa uwanja huo wa Arusha, ambapo wafanyakazi wenyeji si tu kwamba wanajenga alama bali pia wanabadilisha maisha yao wenyewe. Timu ya Mustafa imekuwa na ujuzi zaidi, ikijifunza kutoka kwa wahandisi wa China na kuwa wabobezi wa teknolojia za hali ya juu.

"Mahitaji ya ujenzi wa uwanja ni ya juu zaidi kuliko majengo ya kawaida, kwa hivyo wafanyakazi waliopewa mafunzo hapa wanaweza kushughulikia miradi mbalimbali ya uhandisi," amesema Li Lin, meneja mtendaji wa mradi wa CRCEG. Sauti yake ilikuwa tulivu lakini thabiti, ikijumuisha nidhamu ambayo imekuwa ikiongoza mradi huo kupitia changamoto.

Ukiwa utakuwa moja ya viwanja vya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, uwanja huo ni zaidi ya kituo cha michezo; ni kielelezo cha dhamira ya Tanzania ya kuandaa matukio makubwa ya kimataifa.

Ukiwa unachukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 142,200, mradi huo utakuwa na uwanja wenye viti 30,000 ukiwa na skrini za LED, mfumo wa taa wenye kutumia nishati kiufanisi, na teknolojia za kisasa kwa kukata tiketi na usimamizi. Ukiwa umehamasishwa na madini ya bluu ya Tanzanite yanaopatikana Tanzania pekee na Mlima Kilimanjaro, muundo wa uwanja huo unajumuisha rangi za bendera ya Tanzania, ambayo ni ishara ya fahari ya taifa.

Kwa Zhang Zhewei, mhandisi kijana wa China ambaye amehitimu chuo kikuu punde, uwanja huo ni vyote mradi na safari ya kujiendeleza. Alijiunga na timu ya ujenzi karibu mwaka mmoja uliopita, akifanya upigaji picha wa droni na kuzunguka kupitia idara tofauti za kiufundi ili kujifunza kutoka kila pembe.

"Wakati AFCON itakapoanza hapa 2027, simulizi hizi za ujenzi zitakuwa kumbukumbu zisizoweza kusahaulika, zenye kusisimua kama tu ilivyo michezo yenyewe," Zhang amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha