

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Vijana Chipukizi wa China
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Vijana Chipukizi wa China (CYP), ambao umefunguliwa jana Jumanne mjini Beijing.
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesisitiza katika barua hiyo kwamba CYP wanapaswa kufuata Chama na kuandaa wajenzi wanaofuata matakwa ya mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China.
Wakati Siku ya Kimataifa ya Watoto ikikaribia, Rais Xi ametoa salamu zake kwa watoto kote nchini China, akisema kuwa watoto wanawakilisha nguvu ya siku za baadaye katika kujenga nchi yenye nguvu na kustawisha Taifa la China.
Amevihimiza vikosi vya vijana chipukizi kuelimisha na kuongoza vijana chipukizi kufanya juhudi za kuwa vijana wa mfano wa kuigwa wa zama mpya wa kupenda Chama na nchi, kufanya bidii katika masomo yao na kujiendeleza katika mambo yote.
Rais Xi ametoa wito wa kujenga mazingira mazuri kwa ukuaji mzuri wa watoto.
Cai Qi, Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Shi Taifeng, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya Kamati Kuu ya CPC, alisoma barua hiyo ya Rais Xi kwenye mkutano huo na kutoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC.
Amehimiza vijana wachipukizi kutilia maanani mafundisho ya Rais Xi na kuwa tayari kuchangia kujenga nchi yenye nguvu na kustawisha Taifa la China.
Watu takriban 3,000 walihudhuria mkutano huo.
Cai Qi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, akihudhuria kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Vijana Chipukizi wa China (CYP) mjini Beijing, Mei 27, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
Shi Taifeng, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni ya Kamati Kuu ya CPC, akisoma barua ya pongezi ya Rais Xi Jinping wa China na kutoa hotuba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC kwenye Mkutano Mkuu wa Tisa wa Vijana Chipukizi wa China mjini Beijing, Mei 27, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma