Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kuweka mfano wa uwazi, ushirikiano wa maendeleo na ASEAN na GCC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 28, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa Kilele wa ASEAN (Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki)-China-GCC (Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba) mjini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, Mei 27, 2025. (Xinhua/Rao Aimin)

KUALA LUMPUR - Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipohutubia mkutano wa kwanza wa kilele kati ya Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN), China na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) uliofanyika Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia jana Jumanne, ametoa wito kwa China, ASEAN na GCC kwa pamoja kuweka mfano wa uwazi, ushirikiano wa maendeleo na mafungamano ya ustaarabu wa kuvuka mipaka.

“China, ASEAN na nchi za GCC zina historia ndefu ya mawasiliano ya kirafiki,” Li amesema, akiongeza kuwa dhidi ya mabadiliko magumu katika mazingira ya kimataifa na ukuaji wa uchumi unaodorora, kuanzishwa kwa jukwaa kama hilo la mawasiliano na utaratibu wa ushirikiano kama mkutano huo wa kilele wa pande tatu kunaashiria uvumbuzi mkubwa katika ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda.

Kupitia muunganisho wa miundombinu na ushirikiano wa karibu, Waziri Mkuu huyo wa China amesema, pande hizo tatu zinaweza kujenga mzunguko wa uchumi wenye uhai na nguzo ya ukuaji, ambayo inabeba umuhimu mkubwa kwa ustawi wao vilevile amani na maendeleo ya Asia na dunia.

Li amehimiza pande zote kuchangamkia fursa hii ya kihistoria, kuimarisha kila wakati kiini cha ushirikiano huo wa pande tatu, na kufanya kazi pamoja ili kujenga kielelezo cha ushirikiano na maendeleo duniani.

Amehimiza pande zote kujenga mfano wa kuigwa katika nyanja tatu.

Kwanza, Li ametoa wito kwa pande hizo tatu kujenga mfano wa uwazi wa kuvuka kanda, akisema kwamba idadi ya watu na jumla ya uchumi wa China vilevile ule wa nchi za ASEAN na GCC ni takriban robo moja ya jumla ya dunia.

Pili, ametoa wito kwa pande hizo tatu kujenga mfano wa ushirikiano kati ya nchi zilizoko katika hatua tofauti za maendeleo, akisema kuwa ingawa pande hizo tatu ziko katika hatua tofauti za kimaendeleo, tofauti zao si vizuzi vya ushirikiano bali zinasaidiana kila mmoja.

Tatu, Waziri Mkuu huyo wa China amehimiza pande hizo tatu kujenga mfano wa mafungamano ya ustaarabu wa kuvuka mipaka, akisema kuwa pande hizo tatu ni maskani kwa ustaarabu moto moto na zina thamani ya maadili ya Asia ya amani, ushirikiano, uwazi na ujumuishaji.

Ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na ASEAN na GCC kutekeleza Pendekezo la Ustaarabu Duniani, kuhimiza kufunzana kati ya ustaarabu tofauti na kujenga maafikiano makubwa zaidi na kasi ya amani na maendeleo.

Mkutano huo umepitisha taarifa ya pamoja ya Mkutano wa Kilele wa ASEAN-China-GCC.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa Kilele wa ASEAN (Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki)-China-GCC (Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba) mjini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, Mei 27, 2025. (Xinhua/Rao Aimin)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa Kilele wa ASEAN (Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki)-China-GCC (Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba) mjini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, Mei 27, 2025. (Xinhua/Rao Aimin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha