

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu Li aahidi kuimarisha muunganisho wa kimkakati na ASEAN na GCC kwa ajili ya kujiendeleza kwa pamoja
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia hafla ya ufunguzi wa Baraza la Kiuchumi kati Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN), China na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) 2025 mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Mei 27, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
KUALA LUMPUR - Waziri Mkuu wa China Li Qiang Jumanne wakati akihutubia hafla ya ufunguzi wa Baraza la Kiuchumi kati Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN), China na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC) 2025 amesema kuwa China inapenda kuimarisha muunganisho wa mikakati ya maendeleo na ASEAN na nchi za GCC, kufungua ukurasa mpya kwa ajili ya kujiendeleza kwa pamoja.
"Kufanyika kwa mafanikio kwa Mkutano wa Kilele wa ASEAN-China-GCC kumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa pande tatu," Li amesema, akiongeza kuwa mkutano huo umekuwa na majadiliano ya kina juu ya kaulimbiu ya "Kuwianisha Fursa za Kiuchumi kuelekea Ustawi wa Pamoja," ambayo yalikuwa na umuhimu mkubwa.
Amesema katika dunia ya sasa, kushirikiana kutatua changamoto kwa namna yake ni njia ya kutengeneza fursa.
Katika kukabiliana na kuongezeka kwa migogoro na makabiliano ya siasa za kijiografia, Li amesema, inaaminika kuwa kuendelea kudhamiria katika kuzidisha hali ya kuaminiana na kuimarisha mshikamano kunaweza kuunda fursa za kimkakati za muda mrefu na kufikia maendeleo endelevu na thabiti.
"Katika kukabiliana na kuongezeka kujilinda kibiasharana hali ya upande mmoja, kuendelea kudhamiria kwa ufunguaji mlango zaidi na kuondolewa kwa vizuizi kunaweza kufungua fursa kubwa za soko na kuruhusu nchi zote kunufaika na faida kubwa zaidi kupitia kujenga kwa pamoja soko kubwa zaidi na lenye ujumuishi zaidi," amesema.
Amesisitiza kuwa, katika kukabiliana na hatua zaidi kuelekea kutengana kiuchumi na kuweka vizuizi, kuendelea kudhamiria katika kunufaishana rasilimali na kuwezeshana kunaweza kuunda fursa kwa mageuzi na uboreshaji, vilevile kuongeza ufanisi wa viwanda na kasi ya maendeleo endelevu katika nchi zote.
Li amebainisha kuwa ushirikiano wa kirafiki kati ya China, ASEAN na nchi za GCC una historia ndefu na mizizi mirefu.
Amesisitiza kuwa, China itaendelea kuingiza kasi mpya katika ushirikiano huo wa pande tatu kupitia maendeleo yake yenye sifa bora ya hali ya juu.
Akihutubia hafla ya ufunguzi wa baraza hilo, Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim amesema mkutano wa kwanza wa baraza la ASEAN-China-GCC umetoa taarifa ya pamoja, ukituma ujumbe mzito wa mshikamano na ushirikiano wa pande tatu.
Anwar amebainisha kuwa, China ni mshirika muhimu wa nchi za ASEAN na GCC, ikibeba jukumu muhimu katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi, kudumisha amani na utulivu, na kushikilia haki na usawa wa kimataifa.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia hafla ya ufunguzi wa Baraza la Kiuchumi kati Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN), China na Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba (GCC) 2025 mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Mei 27, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma