

Lugha Nyingine
Moscow kukabidhi mswada wa makubaliano ya amani kwa Kiev hivi karibuni
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova akihudhuria mkutano wa wiki na waandishi wa habari Machi 23, 2023. (Picha ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia)
MOSCOW - Moscow itapeleka mswada wa makubaliano ya amani kwa Kiev hivi karibuni, ambao utaeleza kwa jumla kanuni muhimu za suluhu tarajiwa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova amesema jana Jumanne.
"Russia inaendelea kuandaa mswada wa makubaliano kuhusu mkataba wa amani wa siku za baadaye, ambao utaeleza kwa jumla misimamo kadhaa, zikiwemo kanuni za suluhu, muda wa uwezekano wa makubaliano ya amani, uwezekano wa kusimamisha mapigano," Zakharova amesema katika mkutano wake wa wiki na waandishi wa habari.
Amesema kwamba mara tu mswada huo wa makubaliano utakapokamilika utapeleka kwa Kiev, na Russia inatarajia kuwa Ukraine utaandaa mswada wake kwa kujibu.
Kwenye mazungumzo kwa njia ya simu wiki iliyopita, Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Marekani Donald Trump walikubaliana kwamba Russia itaandaa mswada wa makubaliano unaoelezea masharti ya makubaliano yanayotarajiwa ya amani na Ukraine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma