

Lugha Nyingine
Barabara kuu iliyojengwa na China nchini Saudi Arabia yafunguliwa kwa sehemu
![]() |
Wawakilishi kutoka China Railway 18th Bureau (Saudi Arabia) na Kamisheni ya Kifalme kwa Jubail na Yanbu ya Saudi Arabia wakishiriki kwenye hafla ya ufunguzi wa sehemu ya Barabara Kuu ya Jubail TS-8 mjini Jubail, Saudi Arabia, Mei 27, 2025. (Xinhua/Luo Chen) |
RIYADH - Mradi wa barabara kuu iliyojengwa na Kampuni ya China katika Jimbo la Mashariki la Saudi Arabia, Barabara kuu ya Jubail TS-8, umefikia hatua muhimu jana Jumanne kwa kukabidhiwa sehemu na kufunguliwa kwake kuanza kutumika.
Ikiwa inapatikana katika mji wa Jubail, barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 16.8 na njia sita za kupitisha magari-- iliyojengwa na China Railway 18th Bureau Group (Saudi Arabia) -- inatumika kama muunganisho wa haraka kati ya Barabara kuu ya 95 na Eneo la Viwanda la Jubail katika Jimbo la Mashariki. Sehemu hiyo mpya ya barabara iliyofunguliwa ina urefu wa kilomita 8.1.
Barabara kuu hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kikamilifu na kufunguliwa kuanza kutumika ifikapo Septemba, kampuni hiyo ya China imeeleza.
Mahmoud bin Saleh Al-Theeb, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kifalme mjini Jubail, amesema kufunguliwa kwa barabara kuu hiyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la usafiri mjini Jubail, kuimarisha ufanisi wa usafiri, kunufaisha jumuiya za mitaa, na kuingiza kasi mpya katika maendeleo ya kiuchumi ya kikanda.
Akitambua juhudi kubwa za kampuni hiyo ya China kwenye mradi huo, Al-Theeb amesema suluhu na teknolojia za China zimetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya miundombinu kwa wenyeji.
Cheng Junjie, mwakilishi wa kampuni hiyo ya China, amesema barabara hiyo kuu "inaonyesha ushirikiano wa kina kati ya kampuni yetu na Kamisheni hiyo Kifalme, na ni ushahidi wa urafiki kati ya China na Saudi Arabia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma