

Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini asema uhusiano na Marekani "umerekebishwa" kwa mafaniko
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (mbele) akizungumza kwenye kipindi cha maswali na majibu katika Bunge la Taifa mjini Cape Town, Afrika Kusini, Mei 27, 2025 (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)
CAPE TOWN - Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema jana Jumanne kwamba nchi hiyo "imerekebisha" kwa mafanikio uhusiano wake na Marekani baada ya mkutano wake na Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House wiki iliyopita.
Ramaphosa ametoa kauli hiyo wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Bunge la Taifa huko Cape Town, mji mkuu wa kibunge wa Afrika Kusini.
Ramaphosa amesema ni muhimu kwa kurekebishwa kwa uhusiano, ambao umekuwa na matatizo katika miaka ya hivi karibuni, "hili lilikuwa suala lililochukua mawazo ya watu wengi katika nchi yetu. Tuligundua athari katika uchumi wetu zingekuwa mbaya kama tusingeweza kutengeneza au kurekebisha upya uhusiano."
Rais huyo wa Afrika Kusini alisema, mazungumzo yake ya njia ya simu na Trump – ambayo awali zaidi ni kuhusu mgogoro wa Russia na Ukraine -- yalipelekea uamuzi wa kukutana ana kwa ana.
Ramaphosa amesema kuwa mkutano wa awali na uwepo wa vyombo vya habari ulifuatiwa na mfululizo wa mikutano ya faragha yenye ufanisi.
"Licha ya kile ambacho tuliweza kuona kwenye televisheni, tuliweza kuwa na majadiliano ya maana zaidi na kukutana na Rais Trump na wawakilishi wake katika chumba tulivu ambapo tulikula chakula cha mchana pamoja," amesema.
Ramaphosa ameelezea malengo matatu muhimu ya ziara yake hiyo nchini Marekani, ambayo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kuanzisha upya njia rasmi za mawasiliano kati ya serikali, na kuongeza umuhimu wa nchi hizo mbili katika Mkutano wa Kilele wa Kundi la nchi 20 utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Ameongeza kuwa lengo la nne ni uwezekano wa kuhimiza uwekezaji mkubwa kati ya kampuni za Marekani na Afrika Kusini.
"Tunaamini tumefikia malengo hayo" amesema. "Kuna majadiliano yanayofanyika kuhusu ushuru na uwekezaji, na tunaamini tumeurekebisha uhusiano."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma