

Lugha Nyingine
Timu ya kutokomeza kichocho inayoongozwa na China yamaliza awamu ya 2 ya mradi visiwani Zanzibar
(CRI Online) Mei 28, 2025
Mradi wa kutokomeza kichocho unaoungwa mkono na China umehitimisha kazi yake ya awamu ya pili Kisiwani Pemba, Zanzibar jana Jumanne, licha ya mvua kubwa kunyesha na vikwazo vya vifaa wakati wa msimu wa mvua wa Machi hadi Mei.
Kiongozi wa mradi huo Dai Yang amesema mradi huo uliozinduliwa mapema mwezi Machi, uliendesha duru mbili za utafiti wa magonjwa katika maeneo yenye hatari kubwa na kwamba zaidi ya wakazi 60,000 walichunguzwa na wataalamu 46 wenyeji walipewa mafunzo kwa kutumia vifaa vya lugha ya Kiswahili kuchakata sampuli.
Kwa mujibu wa Dai, mradi huo utahamia Kisiwa cha Unguja katika awamu inayofuata.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma