Mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kati ya China na nchi za Visiwa vya Pasifiki wafikia maafikiano yenye vipengele vitano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza kwa pamoja Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kati ya China na Nchi za Visiwa vya Pasifiki na Rais wa Kiribati ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Taneti Maamau mjini Xiamen, Mkoani Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 28, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameongoza kwa pamoja Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kati ya China na Nchi za Visiwa vya Pasifiki na Rais Taneti Maamau wa Kiribati ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo jana Jumatano mjini Xiamen, Mkoani Fujian, mashariki mwa China akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na nchi za visiwa vya Pasifiki huku akisema kwamba China siku zote imekuwa ikizichukulia nchi hizo kama marafiki, washirika na ndugu wazuri.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wao, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na nchi za Visiwa vya Pasifiki umeonyesha uhai mpya, kupata mafanikio mapya na kufikia ngazi mpya.

Wang ametoa mapendekezo yenye mambo sita kuhusu kujenga jumuiya ya China na nchi za Visiwa vya Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja: kushikilia kuheshimiana, kutoa kipaumbele kwa ushirikiano wa maendeleo, kudumisha utawala unaotilia maanani watu wake, kuhimiza mawasiliano na kufunzana, kulinda haki na usawa, na kudumisha mshikamano katika nyakati zenye changamoto.

Wang amesema, China inaamini kwamba amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana ni machaguo pekee sahihi wakati wa kukabiliwa na mabadiliko makubwa duniani, hali ya sasa na mchakato wa kihistoria.

Mawaziri hao wa mambo ya nje wa nchi za Visiwa vya Pasifiki wameshukuru China kutokana na uungaji mkono wake katika muda mrefu.

Wamesisitiza kuwa ushirikiano kati yao na China umejengwa juu ya msingi wa kuheshimiana, kuaminiana, kuelewana na usawa wa kujitegemea, na kwamba umekuwa uamuzi wa kufanywa kwa kujitegemea wa nchi hizo za visiwa, unaoendana na maslahi yao ya kimsingi, na unasaidia kudumisha amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda.

Wamesisitiza tena dhamira yao ya kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, wakisema kwamba wanatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika ujenzi wa miundombinu, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kujiendeleza bila kuchafua mazingira, kuhimiza kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja kwa sifa bora, na kushirikiana kujenga eneo la Pasifiki lenye amani na ustawi.

Wang amesema kufuatia mazungumzo ya kina juu ya kuimarisha ushirikiano na masuala ya kimataifa na kikanda yanafuatiliwa kwa pamoja, China na nchi za Visiwa vya Pasifiki zimefikia maafikiano kuhusu mambo matano ambayo ni kwamba: Pande zote mbili zinatendeana kwa usawa, pande husika zimedhamiria kuhimiza maendeleo kwa pamoja, na tatu, pande hizo zimekubaliana kudumisha haki na usawa, Nne, pande zote mbili zinakubali kufungua mlango na kushirikishwa na mwisho, zinatetea mawasiliano kati ya ustaarabu mbalimbali.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiongoza kwa pamoja Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kati ya China na Nchi za Visiwa vya Pasifiki na Rais Taneti Maamau wa Kiribati ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje mjini Xiamen, Mkoani Fujian, kusini mashariki mwa China, Mei 28, 2025. (Xinhua/Ding Lin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha