Mjumbe wa Umoja wa Mataifa asema suluhisho la nchi mbili liko mahututi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano juu ya hali ya Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 28, 2025. (Xinhua/Xie E)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano juu ya hali ya Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Mei 28, 2025. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Mjumbe maalum wa muda wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati Sigrid Kaag ameonya jana Jumatano kwamba suluhisho la nchi mbili liko mahututi, akitoa wito wa kuchukua hatua za pamoja ili kulifufua.

"Suluhisho la nchi mbili liko hali ya mahututi. Kulifufua inahitaji hatua za pamoja," amesema Kaag akiongeza kuwa: "Amani haiwezi kuwa biashara au mpango wa muda mfupi. Inahitaji kujengwa juu ya maafikiano ya kimataifa na uhalali, na kuelekea kumaliza mgogoro kutoka kusimamia mgogoro."

Amesema katika Baraza la Usalama kuwa, hakuwezi kuwa na amani endelevu katika eneo la Mashariki ya Kati bila kutatua mgogoro kati ya Israel na Palestina, akiongeza kuwa, mustakabali wa eneo hilo utaendelea kufungamana na mambo yake ya siku za nyuma ambayo hayajatatuliwa, isipokuwa kama tu dhamira thabiti na maamuzi ya kisiasa yatavunja mzunguko huo.

“Kujenga nchi kwa Wapalestina ni haki, si zawadi” amesema.

Amesema, mkutano ujao wa kimataifa wa ngazi ya juu mwezi Juni, utakaoongozwa kwa pamoja na Ufaransa na Saudi Arabia, unatoa fursa muhimu na kwamba haupaswi kuwa zoezi lingine la soga bali ni lazima uanzishe njia kuelekea kukomesha uvamizi huo na kufikia suluhisho la nchi mbili juu ya msingi wa sheria za kimataifa, maazimio ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya awali.

"Tunahitaji kujielekeza wenyewe kutoka kutoa matamko hadi maamuzi. Tunahitaji kutekeleza badala ya kupitisha nyaraka mpya."amesema.

Mjumbe huo wa Umoja wa Mataifa amesema, msaada wa kibinadamu unahitajika kufikia watu wote kote Gaza na kwamba huduma muhimu, mahitaji ya maisha, na heshima ya binadamu vinahitaji kurejeshwa huku kulazimishwa kukimbia makazi kwa raia kukitakiwa kukataliwa na kuepukwa.

Amesema, utawala wa Palestina baada ya vita na mipango mwafaka ya usalama mjini Gaza vinahitajika, wakati huohuo ukamilifu wa ardhi na umoja wa kisiasa wa Gaza na Ukingo wa Magharibi lazima vihifadhiwe na mateka wanapaswa kuachiliwa huru bila masharti.

Ameonya kuwa, wakati Gaza iliyokumbwa na vita inafuatiliwa na dunia nzima, Ukingo wa Magharibi uko kwenye njia hatari.

"Tunahitaji kuchukua hatua sasa kubadili hali ilivyo sasa. Mchakato wa kisiasa uliofafanuliwa vyema, unaoungwa mkono na wengi na wenye ukomo wa muda, unaoandamana na ulinzi na uhakikisho, ni muhimu" amesisitiza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha