

Lugha Nyingine
Viongozi wa kikanda wahimiza makundi yenye silaha nchini DRC kukomesha uhasama
Wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali katika kanda ya Maziwa Makuu wamekutana jana Jumatano nchini Uganda, wakihimiza makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kukomesha uhasama bila masharti.
Wakati wa kuhitimisha Mkutano huo wa 12 wa Ngazi ya Juu wa Mfumo wa Uangalizi wa Kikanda wa Mwongozo wa Amani, Usalama na Ushirikiano (PSC) kwa DRC na Eneo la Maziwa Makuu, limetolewa tamko likihimiza makundi ya kigeni yenye silaha yanayofanya kazi nchini DRC kuweka silaha chini kwa hiari na kujiandaa kurejea katika nchi zao.
Pia wamehimiza nchi wanachama zilizosaini mfumo wa PSC kutimiza ahadi zao za kuheshimu uhuru na ukamilifu wa ardhi wa nchi jirani, na kutohifadhi au kuunga mkono vikundi vyenye silaha au watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu, au vitendo vya mauaji ya kimbari.
Mkutano huo ulioandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebbe, umefanyika wakati kukiwa na hali mbaya ya kisiasa, kibinadamu na kiusalama mashariki mwa DRC.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma