

Lugha Nyingine
Kenya kupunguza utegemezi wa umeme unaotokana na maji ili kuimarisha uhimilivu wa nishati
(CRI Online) Mei 29, 2025
Kampuni ya Umeme ya Kenya (KenGen) imesema inapanga kupunguza utegemezi wa umeme unaotokana na maji nchini humo ili kuimarisha uhimilivu wa nishati, kwa kuwa umeme wa aina hiyo unaweza kuathiriwa na mvua isiyotabirika.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Peter Njenga amesema jana Jumatano kuwa uwezo wa umeme unaotokana na maji nchini Kenya unakadiriwa kuwa megawati 840, ukichukua asilimia 24 ya uzalishaji wa jumla wa umeme.
Kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi, Njenga amesema umeme huo ni chanzo imara cha nishati chenye bei nafuu zaidi, lakini pia kinaweza kuathiriwa kirahisi zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
Ameongeza kuwa kwa vile sasa ukame unaathiri vibaya uzalishaji, utegemezi wa mabwawa ya maji nchini humo unatathminiwa upya.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma