

Lugha Nyingine
Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU apongeza uungaji mkono wa China kwa maendeleo ya Afrika
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf ametoa shukrani za dhati kwa China kutokana na uungaji mkono wake thabiti kwa Kamisheni hiyo na nchi za Afrika katika maeneo muhimu, yakiwemo ya biashara, maendeleo ya miundombinu, kilimo, afya na ujenzi wa uwezo.
Youssouf ametoa kauli hiyo wakati akimuaga Balozi Hu Changchun, mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika.
Amepongeza juhudi za Balozi Hu na kushukuru mchango wa China katika ujenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Afrika, kuunga mkono juhudi za kulinda amani za Afrika, na uungaji mkono katika sekta nyingine muhimu za kijamii.
Wawili hao pia walizungumzia mafanikio ya Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwaka jana mjini Beijing na kusisitiza tena ushirikiano wa kimkakati wa Umoja wa Afrika na China kama mfano wa mshikamano wa pande nyingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma